Kabwili "Bado nipo Yanga SC"

🚨| YUPO YANGA

Kabwili anasema haonekani katika mazoezi na mechi za Yanga kutokana na matatizo yaliyomkuta na kupewa muda wa kupumzika kujiweka sawa kiakili.

Anasema sio kazi rahisi kuweza kuyachukulia kama kawaida na kuishi katika jamii ya binadamu wengine kwani mtu mwingine anaweza kupoteza maisha.

“Naomba niweke wazi leo kupitia heshima ya Mwanaspoti ingawa nafanya jambo la nje ya makubaliano na viongozi wangu bado nipo Yanga, napokea mshahara wangu kwa wakati na posho kama ilivyo kwa wachezaji wengine,” anasema.

“Kiukweli nimeamua kuweka wazi kwa sababu sio jambo dogo viongozi wangu wanalifanya, sipo ndani ya timu kwa maana ya kufanya mazoezi ili nipo kimkataba lakini wananipatia kila kitu kwa wakati.” Mkataba wangu na Yanga umebaki wa miezi minne na mwisho wa msimu huu ndio utamalizika baada ya hapo nitawafuata na kuwauliza wapo tayari kuendelea na mimi au nitafute changamoto mpya sehemu nyingine.”

CHANZO: MWANASPOTI

Post a Comment

0 Comments