Liverpool haitamlipa salah anachotaka kwa sababu yeye ni mwafrika

Mchezaji wa zamani wa Liverpool El-Hadji Diouf kwa utata anamwambia Mohamed Salah klabu hiyo 'haitampa mkataba bora zaidi kwa sababu yeye ni MWAFRIKA'...

Mshambuliaji wa zamani El-Hadji Diouf anamtaka Mohamed Salah kukataa Real Madrid na kusaini mkataba mpya na Liverpool - licha ya madai ya utata pengine Salah hatapata dili analostahili kwa sababu yeye ni Mwafrika.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri unatarajiwa kumalizika mwaka wa 2023 na, licha ya juhudi za Reds za kutaka kumpa mkataba mpya, klabu na mchezaji huyo bado hawajafikia makubaliano.

Hali ya kusita kuongeza mkataba kwa Salah Klabuni hapo imeziweka baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya katika hali ya tahadhari ya kumchukua, vilabu hivyo vikiwemo Real, Barcelona na Juventus..

Cc; Daily Mail Sports 

Post a Comment

0 Comments