SIMBA IKIFUZU ROBO UHAKIKA TIMU NNE.

Ameandika Yassima Sitta Jr.

SIMBA IKIFUZU ROBO UHAKIKA TIMU NNE.

-Watanzania tuna kila sababu ya kuisapoti klabu ya Simba kwenye mchezo wao jumapili April 03 dhidi ya US Gendermarine ya Niger oli Tanzania kujihakikisha kupeleka timu nne tena msimu ujao. 

-Kwanza tunatakiwa kuwashukuru TFF na kocha timu ya taifa Star, Kim Poulsen kwa kukubali ombi la Simba na kuwaruhusu wachezaji saba wa klabu hiyo kujiunga na mazoezi ya timu yao ili kupata muda wa kujiandaa na mchezo huo. 

-Kuna wengine wanalalamika kuwa et Simba wameizalau timu ya Taifa sio kweli mchezo wa Simba ni muhimu zaidi ya ule wa kirafiki wa Tanzania dhidi ya Sudani kesho March 29 hivyo kocha Kim na TFF wako sahihi asilimia 100. 

-Kwa nini Simba ikishinda tutakuwa na uhakika wa kupeleka timu nne msimu ujao (2022/23) Kwa Sasa kwenye ranking ya viwango CAF sisi kama nchi Tanzania tupo nafasi ya 12 tukiwa na pointi zetu 23 iwapo Simba itashida na kufuzu robo tutaongeza pointi 7.5 ambazo tutakuwa na pointi 30.5. 

-Tutakuwa tunapambana na Guinea yenye pointi 31 nafasi ya 09 na imebaki na timu ya Horoya ambayo haiwezi kufuzu robo ya klabu bingwa na timu iyo itatakiwa kushinda kuanzia magoli 2 mchezo mwisho dhidi ya Amazulu ili imalize nafasi ya 3 na Guinea watakuwa na pointi 36 (Hawa tuachane nao) 

-Mshindani wetu kwa sasa ni Libya yenye Pointi 23 kama sisi tupo naye nafasi ya 12 ana timu mbili kombe la shirikisho ambazo ni Ahli Tripoli na Al-Attihad ikiwa Ahli Tripoli imeshafuzu tayari robo huku Al Attihad itatakiwa kupata sare mchezo wa mwisho dhidi ya Orlando Pilates Huku JS Saura yenyewe ikiomba timu hiyo ipoteze na wao washinde dhidi ya Leopards mchezo wa mwisho. 

-Iwapo watashinda au kutoa sare Al Attihad nchi ya Libya itakuwa imefikisha pointi 30.5 kama sisi iwapo Simba itafuzu robo fainali na iwapo Al Attihad hawatafuzu robo Libya itabaki na pointi zao 23 na kuiombea Al Tripoli ifanye vizuri zaidi.

-Nafasi ya 10 ipo Nigeria ambayo ina pointi 26 haina timu yoyote maaana yake pointi zake haziongezeki wala kupungua nafasi ya 11 yupo Zambia ana pointi 24.5 na amebaki na timu moja ya Zanaco nayo imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Pyramids Ugenini. 

-Iwapo Zanaco itashinda Zambia itaiombea CS Sfaxien ya Tunisia ifungwe na Alhi Tripoli ya Libya ili Zanaco imemaliza nafasi ya 3 na pointi za Zambia zitaongezeka na kufika 27 iwapo Simba itakuwa imefuzu robo nchi za Nigeria na Zambia tutakuwa tumezishusha yaani sisi tutakuwa nafasi ya 10 bila kuangalia pointi za wengine.

-Nchi ya Cameroon ipo nafasi ya 14 ina pointi 14.5 na imebakiza timu moja ya Cotton Sports nayo haiwezi kufuzu robo fainali inapambana kumaliza nafasi ya tatu iwapo iitamaliza nafasi ya 3 kwenye msimamo nchi ya Cameron itakuwa na pointi 17 tu ambazo hata 23 ambazo tunazo sasa haiwezi kutufikia.

-Nchi ya Ivory Coast Ina pointi 10.5 na imebaki na timu moja ya Asec Mimosas ili nchi ya Ivory Coastal ituzidi pointi itatakiwa kuiombea Asec Iwe bingwa wa kombe la shirikisho na timu yetu ya Simba isifuzu robo fainali na nchi zingine kama Botswana na Congo Brazzaville nazo zina timu ingawa haziwezi kufuzu robo na haziwezi kutufikia kwa pointi hata timu zao zimalize nafasi ya tatu.

-Watanzania wote hatuna budi ya kuiombea Simba na kuisapoti kwa mbinu zozote zile Ili ifuzu robo fainali ya kombe la shirikisho. Pia Simba yenyewe inatakiwa kuingia uwanjani kwa lengo kushinda kwa mbinu zozote wanatakiwa kushinda..

-Kila la Kheri Simba 
-Kila la kheri Tanzania 


Post a Comment

0 Comments