Simba kucheza saa 4 usiku dhidi ya USGN

- Simba kucheza saa 4 usiku dhidi ya USGN 🇳🇪 imetokana na makubaliano ya klabu zote (4) kwenye kundi (D) Shirikisho (CAF)
.
.
Kwa mujibu wa utaratibu wa (CAF) michezo yote ya mwisho kwenye kundi hasa kama hili ambalo yoyote anaweza kufuzu, mechi zote huchezwa muda mmoja.
.
.
RS Berkane 🇲🇦 ndio waliosababisha mechi hiyo kuchezwa saa (4) usiku. Kutokana na mpishano wa majira Tanzania na Morocco,, Berkane walisema saa (1) ya usiku nchini Tanzania itakuwa ni muda wa kufuturu nchini Morocco, hivyo mechi isogezwe mbele.
.
.
Timu zote zikakubaliana mechi ichezwe saa (4) usiku kwa majira ya Tanzania.
.
.
Kila lakheri Simba sports club, nawatakia ushindi mujarabu kwa Mkapa Jumapili 🙌

Cc; Tom Cruz #binagoupdates

Post a Comment

0 Comments