𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 , 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐙𝐀𝐂𝐇𝐔𝐀𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐌𝐔𝐖𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐊𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐙𝐈
➪Ikiwa imebaki takribani miezi miwili na wiki kadhaa msimu wa 2021/22 kumalizika, klabu vigogo wa soka Tanzania, Yanga na Simba zimeanza kuchuana vikali kuwania wachezaji wa kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu ujao
➪Gazeti la Mwanaspoti limeripoti kuwa Yanga imejitosa kumuwania mshambuliaji wa Asec Mimosas Stephano Ki Aziz, likiwa ni pandekezo la kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi
➪Kulingana na gazeti hilo, Nabi amevutiwa na uwezo wa Ki Aziz katika kupachika mabao na amemuhitaji katika kikosi chake ambacho kina nafasi kubwa ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao
➪Ki Aziz amefunga mabao matatu katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu huu mabao mawili akifunga katika michezo dhidi ya Simba iliyopigwa Dar na Benin
➪Ikumbukwe mabosi wa Simba nao walionyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo baada ya mchezo kati ya Asec Mimosas dhidi ya Simba uliopigwa Benin mwishoni mwa wiki iliyopita
➪Simba iliwasiliana moja kwa moja na Asec kumuulizia mchezaji huyo raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 26
➪Yanga wamezungumza na wakala wa Ki Aziz ambaye pia ni wakala wa mchezaji mwingine wa Yanga, Yacouba Songne,
➪Bado Simba wako Na mazungumzo Mazuri na Wakala wa Ki Aziz na Timu yake Asec Mimosas, Tuendelee kula Mtoli nyama tutazikuta chini.
➪NB:-Timu gani unaipa nafasi kubwa ya kunasa saini ya Mshambuliaji huyo? nasoma Comment..
0 Comments