𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐘𝐀𝐓𝐀𝐉𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐌𝐔𝐖𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐘𝐎𝐓𝐀 𝐎𝐑𝐋𝐀𝐍𝐃𝐎 𝐏𝐈𝐑𝐀𝐓𝐄𝐒

𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐘𝐀𝐓𝐀𝐉𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐌𝐔𝐖𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐘𝐎𝐓𝐀 𝐎𝐑𝐋𝐀𝐍𝐃𝐎 𝐏𝐈𝐑𝐀𝐓𝐄𝐒

➪Nyota wa klabu ya Orlando Pirates, Gabadinho Mhango anahusishwa kuwindwa na mabingwa kihistoria Tanzania, Yanga

➪Muhango aliyeng'ara kwenye michuano ya Afcon 2021 akiwa na timu ya Taifa ya Malawi, amekuwa hana mahusiano mazuri na kocha wa Pirates ambaye anamtuhumu kwa makosa ya utovu wa nidhamu

➪Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa alitamba kuwa klabu hiyo sasa inao uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote ndani ya bara la Afrika

➪Akiwa amewahi kufanya kazi Orlando Pirates, Senzo anatajwa kuwa msimamizi wa usajili huo unaotarajiwa kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga

➪Msimu huu Yanga inalisaka taji la ligi kuu ya NBC baada ya kulikosa kwa misimu minne mfululizo, wakiwania nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao

➪Muhango ni aina ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika akishiriki michuano mikubwa


Post a Comment

0 Comments