𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐘𝐀𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐉𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐀𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐄𝐌𝐀
➪Unapozungumzia timu iliyofanikiwa zaidi hapa Tanzania na pengine ukanda wote wa Afrika Mashariki na kati katika kipindi cha misimu minne iliyopita, Simba ndio klabu ya kwanza kwenye orodha hiyo
➪Katika miaka minne iliyopita Simba imetwaa ubingwa wa ligi kuu mara nne, kombe la FA mara mbili, Ngao ya Jamii mara nne, kombe la Mapinduzi na kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mara mbili
➪Msimu huu wako hatua ya makundi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika na wana nafasi kubwa ya kutinga robo fainali
➪Unajua kwa nini Simba imepata mafanikio haya? Kwa sababu ya ubora wa kikosi chao kilichosheheni nyota wenye umahiri mkubwa. Hilo linachagizwa na umakini wa viongozi wa Simba wakati wa usajili
➪Wakati msimu huu ukiendelea Simba tayari imeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao ambapo mabingwa hao wa Tanzania wanatajwa kukamilisha usajili wa nyota wawili wa Kimataifa mapemaaa
➪Ni Moses Phiri kutoka klabu ya Zanaco Fc ya Zambia na Victorien Adebayor kutoka klabu ya US Gendermerie ya Niger
➪Hivi karibuni Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' alidokeza kuwa Adebayor aliyepachika mabao manne kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, ataitumikia Simba msimu ujao, mazungumzo ya kumsajili yako katika hatua za mwisho
➪Kuhusu Phiri, Mo alisema watatoa taarifa pale mchakato wa usajili wake utakapokamilika ingawa taarifa za uhakika ni kuwa Phiri tayari amesaaini mkataba wa awali kuitumikia Simba msimu ujao
➪Nyota hawa utakuwa usajili wa kwanza wa Simba kuelekea msimu ujao ambao Simba inatarajiwa kuja na malengo makubwa zaidi ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika
0 Comments