𝐖𝐀𝐂𝐇𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐒𝐈𝐓𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐀𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐀𝐓𝐀𝐁𝐀 𝐉𝐔𝐍𝐈



➪Wachezaji sita wa kigeni katika klabu ya Simba wanatarajia kumaliza mikataba yao kwenye klabu hiyo huku kuendelea kubaki au kutobaki kutatokana na ripoti ya Kocha Mkuu, Pablo Franco

➪Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa wachezaji Bernard Morrison, Chris Mugalu, Meddie Kagere, Thadeo Lwanga, Joash Onyango na Paschal Wawa mikataba yao inaelekea ukingoni, huku ikitajwa klabu ipo kwenye mazungumza na baadhi ya wachezaji ambao inataka kuwabakisha.

➪"Tunajua kuna baadhi ya wachezaji wanakaribia kumaliza mikataba yao, lakini tuko kwenye mazungumzo nao, na kubaki au kutoendelea pia kutatokana na ripoti ya mwalimu," alisema Meneja Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally

➪Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Bodi ya klabu, Salim Abdallah 'Try Again', alisema kuwa watasajili wachezaji wanne wa kigeni wenye uwezo wa hali ya juu, ili kukiboresha kikosi hicho na kuwa imara kwenye msimu ujao wa michuano ya kimataifa.

➪Alisema wanatarajia kusajili beki mmoja wa kati, mastraika wawili na winga mmoja.

➪Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kufikia mahali pazuri kwenye usajili ni Victorien Adebayor anayeichezea US Gendamarie ya Niger na Moses Phiri anayechezea Zanaco ya Zambia

➪Simba pia inatajwa kuwa katika mchakato wa kumrejesha kwa mkopo winga Luis Miquissone anayeitumikia Al Ahly


Post a Comment

0 Comments