𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐆𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀𝐌𝐊𝐄𝐑𝐀 𝐌𝐎𝐑𝐑𝐈𝐒𝐎𝐍

𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐆𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀𝐌𝐊𝐄𝐑𝐀 𝐌𝐎𝐑𝐑𝐈𝐒𝐎𝐍

Kiungo mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison ameshangazwa na kiwango duni kilichoonyeshwa na washambuliaji wa timu ya Taifa ya Ghana katika mchezo wa play-off kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Nigeria

➪Mchezo huo uliopigwa jana huko Ghana, ulimalizika kwa suhulu ya bila kufungana

➪Morrison amewatuhumu maafisa wa soka huko Ghana kuwa wamekuwa wakichagua timu ya Taifa kwa upendeleo hivyo kupelekea timu hiyo haifanyi vizuri kwenye michuano ya Kimataifa

➪"Fikiria unapuuzwa kwa sababu ya hawa washambuliaji wanashusha daraja la ligi unayocheza kwa sababu wengine walipata nafasi na bahati ya kuwa katika ligi kubwa za ulaya na vilabu vya nje ya Afrika"

➪"Wameifanya timu ya Taifa ya Ghana kuwa kama biashara ya kifamilia. Je, ni kitu gani cha kipekee ambacho wanacho hawa washambuliaji kinachofanya sisi tusiweze kuwakilisha taifa?"

➪"Unadharau ligi za afrika lakini unawaita wachezaji wa ligi ya Ghana kwenye timu ya taifa ambao hata hawachezi ligi ya mabingwa"

➪"Kuna wakati ukweli lazima usemwe, nilichagua jezi namba 3 kwasababu ya ASAMOAH GYAN, kwangu ndiye mshambuliaji bora niliyemtazama na kunivutia tangu utotoni, naamini yeye ni bora katika nyanja zote, lakini nisitambulike kati ya hawa washambuliaji waliopo?"

➪"Kwa hawa Washambuliaji tunaowaita kwenye timu ya taifa ni bora kuzingatia majukumu yangu Simba Sc na kusahau hili, timu nyingi za taifa za Afrika huwapa nafasi wachezaji wa ligi ya ndani na hata ndani ya afrika lakini Ghana haiko hivyo, watakutambua kama una watu wanaokubeba"

➪"Nilichezea AS Vita, Orlando Pirates, Yanga Sc na sasa nipo kwenye klabu kubwa zaidi Tanzania Simba Sc, lakini sikuwahi kutambulika kwasababu sina rafiki huko. Ligi ya Tanzania sio nzuri hivyo sawa, lakini inawezekanaje kuita wachezaji wawili kutoka Azam Fc ambayo hao hao wachezaji uliowaita kila wakati wanafungwa na Simba Sc?"


Post a Comment

0 Comments