𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐊𝐔𝐈𝐍𝐆𝐈𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐁𝐈𝐍𝐈 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐏𝐈𝐋𝐈

𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐊𝐔𝐈𝐍𝐆𝐈𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐁𝐈𝐍𝐈 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐏𝐈𝐋𝐈

➪Mabingwa wa nchi Simba wanatarajiwa kuingia kambini siku ya kesho Jumapili kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya USGN ambao utapigwa April 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

➪Simba itakuwa na takribani wiki moja kukamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo muhimu kwenye michuano ya kombe la Shirikisho

➪Tiketi kuelekea mchezo huo zilianza kuuzwa siku ya jana ambapo CAF imeruhusu mashabiki 35,000 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, wakikataa maombi yaliyowasilishwa na uongozi wa Simba kuomba ongezeko la mashabiki 10,000

➪Meneja wa habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wataingia kambini hapo kesho, wanahitaji kuzitumia vyema siku zilizobaki kuelekea mchezo huo

➪Simba inahitaji kupata ushindi dhidi ya USGN ili kujihakikishia kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Post a Comment

0 Comments