𝐌𝐀𝐉𝐄𝐑𝐀𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐙𝐈𝐃𝐈 𝐊𝐔𝐌𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀 𝐇𝐀𝐙𝐀𝐑𝐃

𝐌𝐀𝐉𝐄𝐑𝐀𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐙𝐈𝐃𝐈 𝐊𝐔𝐌𝐔𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀 𝐇𝐀𝐙𝐀𝐑𝐃

➪Tangu aliposajiliwa na Read Madrid akitokea Chelsea Fc, mshambuliaji Eden Hazard ametumia muda mwingi nje ya uwanja akiuguza majeraha

➪Jana klabu ya Real Madrid ilithibitisha kuwa Hazard anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kutibu jeraha la kifundo cha mguu

➪"Mchezaji wetu Eden Hazard atafanyiwa upasuaji siku chache zijazo ili kuondoa sahani ya osteosynthesis kwenye fibula yake ya kulia," taarifa kutoka Madrid ilibainisha

➪Hazard anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi baada ya upasuaji huo uliolenga kuondoa ute uliopo kwenye fibula yake ya kulia kuanzia Machi 2020

➪Hazard alisajiliwa na Real Madrid mwaka 2019, akitokea klabu ya Chelsea Fc. Amewatumikia katika michezo 65 tu mabingwa hao kihistoria barani Ulaya kutokana na mfululizo wa majeraha

➪Amekuwa akihusishwa kutaka kurejea Uingereza kujiunga na timu yake ya zamani, Chelsea Fc


Post a Comment

0 Comments