Daktari kutoka nchini Zambia, Joseph Kabungo ambae jana alikuwa ofisa wa CAF katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia baina ya Nigeria vs Ghana amepoteza maisha.
Chanzo cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Nigeria mara baada ya mchezo huo kuisha kwa sare ya 1-1 na
Ghana kufanikiwa kufuzu kombe la Dunia.
Kutokana na vyanzo mbalimbali vinaripoti kuwa tukio hilo lilitokea wakati mashabiki wa Nigeria wakifanya vurugu za kulazimisha kuvamia ndani ya eneo la kuchezea, kitu kilichompelekea apoteze fahamu na baadae kufariki licha ya juhudi mbalimbali kufanyika kuokoa maisha yake.
Credit: African Football Greats.
0 Comments