HALI MBAYA KWA TSC QUEENS.

🚨| HALI MBAYA KWA TSC QUEENS.

Klabu ya TSC Queens ya Jijini Mwanza inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) imekwama jijini hapa kutokana na kutokuwa na fedha za kuifikisha Jijini Dar es salaam kucheza na Yanga Queens Machi 30 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Michael John ameiambia Mwanaspoti walifika jana mchana Jijini Dodoma na kucheza jioni hali ambayo imechangia kupoteza dhidi ya Fountain Gate Princess kwa mabao 7-0.

Amesema wamefikia katika Nyumba ya wageni ya Kijoti iliyopo jirani na uwanja na hawajui wataamkaje kwani hawana hata fedha ya chakula.

Alisema wanatakiwa kwenda Jijini Dar es salaam lakini hawana fedha za kuwafikisha huko.

"Hata jezi leo tumepewa na Fountain Mara baada ya kufanana maana tuna seti moja tu. Shime shime tunaomba msaada hali yetu ni mbaya," amesema.

Meneja wa timu hiyo,Frank Philipo amesema wanaukata wa hali ya juu na ilibidi mchana watafute sehemu ya bei rahisi ili wachezaji waweze kula.

"Tumekula saa nane tumecheza saa 10 jioni tumesafiri leo tumecheza leo, hata maji yakunywa yalikuwa ya shida," amesema

Post a Comment

0 Comments