-Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Pablo Franco Martin amesema kuwa amepeleka maombi kwa kocha wa timu ya Taifa Stars, Kim Poulsen na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuwaomba wawaondoe wachezaji saba wa Simba kwenye kambi ya Timu ya Taifa.
-Kocha Pablo amedai kuwa Simba wana mechi ngumu ambayo ndio fainali kwao dhidi ya US Gendermarine kwa ajili ya kufuzu robo fainali ya kombe la shirikisho hivyo wachezaji hao wanatakiwa kupumzika ili kuweka miili yao fiti kwa ajili ya mapambano ya mchezo huo wa April 03.
-Wachezaji 7 wa Simba (Aishi Manula, Israel Mwenda, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude na Kibu Denis) wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kirafiki kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Afrika ya Kati leo March 23, dhidi ya Botswana March 26 na dhidi ya Sudani March 29.
Credit-Yossima Sittajr
0 Comments