Kiungo mshambuliaji wa Simba Sc Hassan Dilunga bado anaendeleza kuuguza majeraha ya goti aliyopata mwezi uliopita na anaweza kuwa nje mpaka mwishoni mwa msimu
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Dilunga bado anaendelea na matibabu pengine msimu huu hatashiriki kuukamilisha
"Ni kweli, Dilunga bado ni mgonjwa na pengine anaweza asionekane kabisa katika mechi zilizobaki msimu huu kutokana na kuumia goti na uongozi unafanya utaratibu wa kumfanyia upasuaji," alisema Ahmed|
0 Comments