UJUMBE WA BERNARD BAADA YA GHANA KUTOKA SARE YA BILA KUFUNGANA NA NIGERIA


"Fikiria unapuuzwa kwa sababu ya hawa washambuliaji🤦🏽‍♂️wanashusha daraja la ligi unayocheza kwa sababu wengine walipata nafasi na bahati ya kuwa katika ligi kubwa za ulaya na vilabu vya ya nje ya Afrika😏 

Wameifanya timu ya Taifa ya Ghana kuwa kama biashara ya kifamilia. 

Je, ni kitu gani cha kipekee ambacho wanacho hawa washambuliaji kinachofanya sisi tusiweze kuwakilisha taifa? Unadharau ligi za afrika lakini unawaita wachezaji wa ligi ya Ghana kwenye timu ya taifa😏 ambao hata hawachezi ligi ya mabingwa🤦🏽‍♂️

"Kuna wakati ukweli lazima usemwe, Nilichagua jezi namba 3 kwasababu ya ASAMOAH GYAN, kwangu ndiye mshambuliaji bora niliyemtazama na kunivutia tangu utotoni, naamini yeye ni bora katika nyanja zote, lakini nisitambulike kati ya hawa washambuliaji waliopo? " 

"Kwa hawa Washambuliaji tunaowaita kwenye timu ya taifa😂 ni bora kuzingatia majukumu ya @simbasctanzania na kusahau hili🤦🏽‍♂️, timu nyingi za taifa za Afrika huwapa nafasi wachezaji wa ligi ya ndani na hata ndani ya afrika lakini Ghana haiko hivyo, watakutambua kama una watu wanaokubeba"

"Nilichezea AS Vita, Orlando Pirates, Yanga Sc na sasa nipo kwenye klabu kubwa zaidi Tanzania Simba Sc, lakini sikuwahi kutambulika kwasababu sina rafiki huko😏.

"Ligi ya Tanzania sio nzuri hivyo sawa, lakini inawezekanaje kuita wachezaji wawili kutoka Azam Fc ambayo hao hao wachezaji uliowaita kila wakati wanafungwa na Simba Sc?" 

Ngoja niishie hapa ila nipo tayari kumsikiliza Mghana yeyote ambaye anadhani ana mawazo tofauti na haya" 

Cc officialfelixtz.

Post a Comment

0 Comments