𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐒𝐎𝐊𝐀 𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐂𝐀, 𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐍𝐈 𝐁𝐑𝐀𝐍𝐃 - 𝐍𝐃𝐔𝐌𝐁𝐀𝐑𝐎
➪Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro amesema Serikali imenufaika kwa kiasi kikubwa na udhamini walioweka katika klabu ya Simba kupitia nembo ya Visit Tanzania
➪Dk Ndumbaro amesema kwa mujibu wa takwimu za CAF, Simba ndio klabu inayotizamwa zaidi barani Afrika ambapo takribani mashabiki Mil 500 huwaangalia kupitia TV
➪"Kwa hapa ndani tunaweza kubishana, lakini katika soka la Afrika, Simba ni brand. Huko nje thamani ya klabu ya Simba ni kubwa kuliko klabu yoyote Tanzania. Mechi moja ya Simba inatazamwa na mashabiki zaidi ya Mil 500. Kwa mechi sita walizocheza, zaidi ya mashabiki Bil 3 wameiona nembo ya Visit Tanzania. Tunaweza kupata angalau asilimia 1 tu ya hao kuja kutalii"
➪"Tuliwapa Yanga nao watangaze Visit Kilimanjaro and Zanzibar lakini kilichotokea wao walitolewa asubuhi tu," alisema Dk Ndumbaro.
0 Comments