FIFA inapanga kuongeza muda wa mechi za Kombe la Dunia la FIFA, Qatar 2022 kutoka dakika 90 hadi dakika 100.
Katika miezi ya hivi karibuni FIFA wamepata shutuma nyingi baada ya kutaka kufanya Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya miaka miwili badala ya kila miaka minne.
Kwa nchi nyingi na mashabiki hiyo ni nyingi mno, ingawa wazo hilo limekuwa na uungwaji mkono kutoka sehemu fulani duniani ambao wangekaribisha nafasi zaidi za kufuzu.
Sasa shirikisho la kandanda duniani linahatarisha kurudi nyuma zaidi kwa mipango yao ya mashindano hayo, huku wakiangalia kuanzishwa kwa mechi za dakika 100 kwa msimu huu wa baridi huko QATAR
Kulingana na Corriere dello Sport, kupitia Football Italia, FIFA wanatazamia kuongeza muda wa mechi kwa dakika 10, ili kuakisha zile dakika za zamani, za 90 zinakamilika haswa
Masuala yanakuja kutokana na ukweli kwamba mpira haubaki kucheza kwa muda mrefu katika mechi za soka, kwa hakika si muda mrefu kama inavyotarajiwa.
Kulingana na CIES Football Observatory, mpira unasalia tu kuchezwa kwa 64.7% ya mechi katika Ligi ya Mabingwa, na idadi hiyo inashuka hadi 62% tu katika Ligi Kuu EPL ( yani muda husika unaotakiwa kutumiwa mpira kuchezwa)
FIFA inatumai kuboresha muda ambao mchezo unachezwa kwa kuongeza dakika 10 za ziada, ingawa hazitaboresha asilimia.
Wazo hilo linasemekana kuwa limetoka moja kwa moja kutoka kwa rais wa FIFA Gianni Infantino, ambaye urais wake unatazamiwa kuendelea hadi mwaka ujao, ambapo anaweza kugombea tena kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Siku za nyuma ilipendekezwa kuwa mpira wa miguu utumie mfumo wa saa unaofanana na ule wa mchezo wa rugby, ambapo saa husimamishwa kwa ajili ya mapumziko, majeraha na muda wanaotumia wachezaji kutoka na kuingia ndani ya uwanja, yani Sub ili ule muda utumiwe kikamilifu.
Pamoja na michuano ya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili na dakika 10 kwa mechi nyingi zaidi, FIFA wanatazamiwa kutambulisha timu zaidi kwenye michuano yao, huku toleo la 2026 nchini Marekani, Mexico na Canada kushirikisha timu 48 kwenye fainali kwa mara ya kwanza..
Via Sport bible
0 Comments